MGUNDUZI KUTOKA TANZANIA
MPEMBA EFFECT “MAJI ya moto yaliyochemka yanaganda (kuwa barafu) haraka zaidi kabla ya maji ya baridi” . ERASTO UPANDE WA KUSHOTO AKIWA NA DR.OSBORNE Ni ugunduzi wa kisayansi wa Mtanzania usiotajwa kwenye Vitabuni, Shuleni wala Vyuoni mwetu hapa nchini, lakini ni gumzo la kitaaluma katika Vyuo na taasisi mbalimbali za elimu za Mataifa mbalimbali. Ni “Udhani” (Hypothesis) unaoumiza vichwa vya wanasayansi wa Dunia yote, kuanzia Ulaya Magharibi, Amerika mpaka Asia. Ugunduzi huu wa kisayansi unaeoelezea “sifa ya kipekee ya maji” ulifanywa na mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Kitanzania katika shule ya sekondari Magamba, Lushoto, Mkoani Tanga, mwaka 1963. Jina la Mwanafunzi huyo ni Erasto Bartholomeo Mpemba, jina ambalo sifa hiyo ya maji (physical phenomenon) imepewa, yaani “Mpemba effect”. Erasto Batholomeo Mpemba, kama ilivyokuwa kwa wanasayansi wengine maarufu duniani, alifanikiwa kugundua sifa hii muhimu ya maji kama ajali tu (accidental discovery), kama ilivyokuwa kw...