Posts

Showing posts from March 29, 2023

JINSI YA KUMLINDA MTOTO WAKO DHIDI YA UKATILI.

Image
JINSI YA KUMLINDA MTOTO WAKO DHIDI YA UKATILI. Hakuna mzazi ambaye anapenda mtoto wake afanyiwe ukatili,lakini katika dunia hii ambayo tunaishi matukio ya ukatili yamekithiri sana,na kwa bahati mbaya sana yanafanyika kwa watoto,je kama wazazi au jamii tunatakiwa tufanye nini kumlinda mtoto dhidi ya ukatili? FATILIA KWA UKARIBU WATU AMBAO WANAKUWA KARIBU NA MWANAO (MARAFIKI AU NDUGU). Jaribu kufatilia tabia za  watu wa karibu na mwanao,je tabia zao zinaweza kumuathiri mtoto wako kwa namna gani,je tabia zao zinaweza kupelekea tukio la ukatili kwa mtoto wako,na kama unaona kuna tabia au viashiria ambavyo sio vizuri kwa mwanao,mweke mwanao mbali na watu hao. FATILIA KWA UKARIBU MICHEZO AMBAYO MWANAO ANACHEZA. Mara nyingi mtoto hucheza michezo ambayo ameizoea au mchezo mpya,fatilia sana michezo anayocheza akiwa mwenyewe na akiwa na wenzake,katika michezo hiyo utagundua kitu au utajifunza kitu kutoka kwa mwanao kipi kinaendelea kwake.Lakini pia unaweza ukagundua hatari ambayo mwanao anaw...