RAIS DOKT POMBE JOHN MAGUFULI
LEO NAKULETEA HISTORIA YA RAIS WETU DKT MAGUFULI NA WASIFU WAKE Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita). Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Elimu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974. Pia alijiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Seminari Katoke-Biharamulo na Lake Sekondari-Mwanza kati ya mwaka 1975 hadi 1978. Aidha, mwaka 1979 hadi 1981 aliendelea na masomo yake ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Mkwawa Mkoani Iringa. Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza. Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1981 – 1982, alisoma di...