Posts

Showing posts from January, 2017

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016/2017 YAMETOKA

Image
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016 BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 31, 2017 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Sekondari, Kidato cha Nne kwa mwaka 2016, mtihani ambao ulifanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.44 ukilinganishwa na ule wa mwaka jana. Katika matokeo hayo, shule za Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam zimeonekana kung’ara zaidi kwa kushika nafasi za juu wakati huohuo shule 6 za Dar es Salaam zikishika nafasi 10 za mwisho katika matokeo hayo. SHULE ZILIZOINGIA 10 BORA KITAIFA: Feza Boys Sec School – Dar es Salaam St. Francis Girls Sec School -Mbeya Kaizirege Junior Sec School – Kagera Marian Gilrs Sec School – Pwani Marian Boys Sec School- Pwani St. Aloysius Girls Sec School – Pwani Shamsiye Boys Sec School – Dar es Salaam Anuarite Girls Sec School- Kilimanjaro Kifungilo Girls Sec School- Tanga Thomas More Machrina Sec School – Dar es Salaam SHULE ZA DAR ES SALAAM ZILIZOSHIK...

MGUNDUZI KUTOKA TANZANIA

Image
MPEMBA EFFECT “MAJI ya moto yaliyochemka yanaganda (kuwa barafu) haraka zaidi kabla ya maji ya baridi” . ERASTO UPANDE WA KUSHOTO AKIWA NA DR.OSBORNE Ni ugunduzi wa kisayansi wa Mtanzania usiotajwa kwenye Vitabuni, Shuleni wala Vyuoni mwetu hapa nchini, lakini ni gumzo la kitaaluma katika Vyuo na taasisi mbalimbali za elimu za Mataifa mbalimbali. Ni “Udhani” (Hypothesis) unaoumiza vichwa vya wanasayansi wa Dunia yote, kuanzia Ulaya Magharibi, Amerika mpaka Asia. Ugunduzi huu wa kisayansi unaeoelezea “sifa ya kipekee ya maji” ulifanywa na mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Kitanzania katika shule ya sekondari Magamba, Lushoto, Mkoani Tanga, mwaka 1963. Jina la Mwanafunzi huyo ni Erasto Bartholomeo Mpemba, jina ambalo sifa hiyo ya maji (physical phenomenon) imepewa, yaani “Mpemba effect”. Erasto Batholomeo Mpemba, kama ilivyokuwa kwa wanasayansi wengine maarufu duniani, alifanikiwa kugundua sifa hii muhimu ya maji kama ajali tu (accidental discovery), kama ilivyokuwa kw...

WATU WALIOWAHI KUTEMBEA MWEZINI

Image
Neil Armstrong (1930 - 2012)  na  Edwin 'Buzz' Aldrin ( alizaliwa  1930) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Armstrong ni maarufu sana kwa maneno yake baada ya kuwa mtu wa kwanza kuukanyaga Mwezi: "Hatua moja ndogo kwa mwanamume mmoja, hatua moja kubwa kwa binadamu." Buzz Aldrin alimfuata. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Wakiwa kwenye Mwezi, Neil na Buzz waliweka bendera ya Marekani na kuacha bango lililokuwa na ujumbe, "Hapa, wanaume kutoka sayari ya Dunia walikanyaga Mwezi kwa mara ya kwanza Julai 1969, AD (Baada ya Kuzaliwa kwa Yesu). Tulifika sote hapa kwa amani kwa niaba ya binadamu wote." Charles 'Pete' Conrad (1930 - 1999) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Apollo 12 ilipaa angani kukiwa na tufani na radi, hali iliyosababisha nguvu za umeme kuzimika muda mfupi baada yao kuruka angani. Conrad mwishowe alipoukanyaga Mwezi, alisema kwa sauti: "Whoopee! Bwana, hiyo huenda ilikuwa hatua ndogo kwa Neil, lakini kwangu imekuwa ku...

RAIS DOKT POMBE JOHN MAGUFULI

Image
LEO NAKULETEA HISTORIA YA RAIS WETU DKT MAGUFULI NA WASIFU WAKE Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita). Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Elimu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipata elimu ya msingi  katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974. Pia alijiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Seminari Katoke-Biharamulo na Lake Sekondari-Mwanza kati ya mwaka 1975 hadi 1978. Aidha, mwaka 1979 hadi 1981 aliendelea na masomo yake ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Mkwawa Mkoani Iringa. Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza.  Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.  Mwaka 1981 – 1982, alisoma di...