JINSI YA KUMLINDA MTOTO WAKO DHIDI YA UKATILI.


JINSI YA KUMLINDA MTOTO WAKO DHIDI YA UKATILI.


Hakuna mzazi ambaye anapenda mtoto wake afanyiwe ukatili,lakini katika dunia hii ambayo tunaishi matukio ya ukatili yamekithiri sana,na kwa bahati mbaya sana yanafanyika kwa watoto,je kama wazazi au jamii tunatakiwa tufanye nini kumlinda mtoto dhidi ya ukatili?

FATILIA KWA UKARIBU WATU AMBAO WANAKUWA KARIBU NA MWANAO (MARAFIKI AU NDUGU).

Jaribu kufatilia tabia za  watu wa karibu na mwanao,je tabia zao zinaweza kumuathiri mtoto wako kwa namna gani,je tabia zao zinaweza kupelekea tukio la ukatili kwa mtoto wako,na kama unaona kuna tabia au viashiria ambavyo sio vizuri kwa mwanao,mweke mwanao mbali na watu hao.

FATILIA KWA UKARIBU MICHEZO AMBAYO MWANAO ANACHEZA.

Mara nyingi mtoto hucheza michezo ambayo ameizoea au mchezo mpya,fatilia sana michezo anayocheza akiwa mwenyewe na akiwa na wenzake,katika michezo hiyo utagundua kitu au utajifunza kitu kutoka kwa mwanao kipi kinaendelea kwake.Lakini pia unaweza ukagundua hatari ambayo mwanao anaweza akaipata kutokana na michezo hiyo.



MFUNDISHE/WAFUNDISHE KULINDA SEHEMU ZAO ZA SIRI.

Mfundishe mtoto wako kulinda sehemu zake za siri kwa asilimia mia moja , yeye ndie anahusika kulinda sehemu zake za siri,mtoto yeye ndio mmiliki wa mwili wake asilimia mia 100,asiruhusu mtu aushike mwili wake hovyo,mwili wake una thamani sana,lakini pia asiruhusu mtu ampige picha au video akiwa uchi au nusu uchi,kwani watu wanatumia picha na video hizo kuzisambaza mtandaoni.


MPE MWANAO MAJIBU SAHIHI.

Watoto wanakuwa na maswali wanayojiuliza sana vichwani mwao,moja ya vitu hivyo ni vitu vinavyohusiana na maumbile yao,Lakini pia wanakuwa na maswali kuhusiana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika miili yao,pale wanapokuuliza maswali kama hayo unapaswa kumpa majibu sahihi yatakompa uwelewa kujihusu yeye mweneywe.

ONGEA NA MWANAO KUHUSIANA NA MATUKIO YA UKATILI.

Moja ya vitu ambavyo mzazi anatakiwa avifanye kwa mwanane ni kuongea na mwanae kuhusiana na mambo yanahusiana na ukatili,ni lazima mzazi aongee na mwanae kuhusiana na viasharia mbalimbali vya ukatili,nini cha kufanya anapohisi hatari,mazingira yapi yatamfanya aingie kwenye ukatili,na madhari yapi atayapata atakapofanya au kufanyiwa ukatili,mambo hayo yatamsadia mtoto kuwa na uwelewa  wa jinsi ya kukabiliana na ukatili.

MFUNDISHE MWANAO KUTOA TAARIFA ANAPOHISI HATARI.

Wazazi wengi hawana mahusiano ya karibu na watoto wao hivyo kukosa mazungumzo na watoto wao,hata anapokuwa na changamoto inayomsumbua anashindwa aiwasilishe vipi kwa mzazi wake,hivyo wazazi wakae karibu na watoto wao na wawafundishe kutoa taarifa pale wanapohisi hatari fulani pale  inawajilia,na mzazi fatilia kwa ukaribu taarifa ambazo mtoto wako anakupatia.


PITIA VITABU,PICHA NA VIDEO ANAVYOSOMA NA KUTAZAMA MTOTO WAKO.

Siku hizi kuna vitabu,picha na video ambazo zinachochea ukatili,vitabu na video hizo zinamfanya mtoto aone kuwa vitendo vya ukatili sio vibaya kwake,na baadhi vinamshawishi mtoto kufanya vitendo hivyo,hivyo unapompa au unamkuta mwanao anasoma kitabu,jarida au gazeti jarfibu kupitia kwanza kujua maudhui yaliyopo ndani ya vitabu hivyo sambamba na hivyo pitia pia picha na video ambazo anaziangalia kujua maudhui yaliyomo katika picha na video hizo.

CHUNGUZA MABADILIKO YA MWANAO MARA KWA MARA.

Mzazi unatakiwa uwe makini na kugundua kila badiliko la tabia ya mwanao,jaribu kufatailia kipi kimesabababisha badiliko la tabia kwa mwanao, katika mabadiliko hayo ndipo unaweza ukajua kipi kinaendelea kwa mwanao.Pindi unapogundua mabadiliko yoyote kwa mwanao tafuta kujua nini kimesababisha mabadiliko hayo,na pia angalia kama mabadaliko hayo ni chanya au hasi katika  ukuaji wake.Kwa namna hiyo unaweza ukamlinda mtoto wako dhidi ya ukatili.

Kumbuka mzazi unahusika kwa asilimia mia moja katika kumlinda mtoto wako dhidi ya ukatili,Mzazi ni mtu ambae anaaminiwa sana na mtoto hivyo ukimpa msingi mzuri  wa malezi na miongozo basi anaweza ukamlinda dhidi ya ukatili.

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016/2017 YAMETOKA

WATU WALIOWAHI KUTEMBEA MWEZINI